Mhubiri 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 6 (Swahili) Ecclesiastes 6 (English)

Kuna baa nililoliona mimi chini ya jua, nalo linawalemea wanadamu kwa uzito; Mhubiri 6:1

There is an evil which I have seen under the sun, and it is heavy on men:

mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya. Mhubiri 6:2

a man to whom God gives riches, wealth, and honor, so that he lacks nothing for his soul of all that he desires, yet God gives him no power to eat of it, but an alien eats it. This is vanity, and it is an evil disease.

Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo; Mhubiri 6:3

If a man fathers a hundred children, and lives many years, so that the days of his years are many, but his soul is not filled with good, and moreover he has no burial; I say, that an untimely birth is better than he:

yaani, hiyo huja katika ubatili, na huenda gizani, nalo jina lake limefunikwa giza; Mhubiri 6:4

for it comes in vanity, and departs in darkness, and its name is covered with darkness.

tena, haikuliona jua wala kulifahamu; basi, hii imepata kustarehe kuliko yule; Mhubiri 6:5

Moreover it has not seen the sun nor known it. This has rest rather than the other.

naam, ajapoishi miaka elfu mara mbili, asijiburudishe kwa mema; je! Wote hawaendi mahali pamoja? Mhubiri 6:6

Yes, though he live a thousand years twice told, and yet fails to enjoy good, don't all go to one place?

Kazi yote ya binadamu ni kwa kinywa chake, Walakini hata hivyo nafsi yake hashibi. Mhubiri 6:7

All the labor of man is for his mouth, and yet the appetite is not filled.

Kwa maana mwenye hekima hupata faida gani kuliko mpumbavu? Au maskini ana nini kuliko yeye ajuaye kwenda mbele ya walio hai? Mhubiri 6:8

For what advantage has the wise more than the fool? What has the poor man, that knows how to walk before the living?

Heri kuona kwa macho, Kuliko kutanga-tanga kwa tamaa. Hayo nayo ni ubatili, na kujilisha upepo. Mhubiri 6:9

Better is the sight of the eyes than the wandering of the desire. This also is vanity and a chasing after wind.

Na awe kitu cho chote, aliitwa jina lake zamani za kale, naye amejulikana kuwa ndiye mwanadamu; wala hawezi kabisa kushindana na yeye aliye na uwezo kuliko yeye mwenyewe. Mhubiri 6:10

Whatever has been, its name was given long ago; and it is known what man is; neither can he contend with him who is mightier than he.

Basi, kwa kuwa kuna mambo mengi yaongezayo ubatili, mwanadamu hufaidiwa nini? Mhubiri 6:11

For there are many words that create vanity. What does that profit man?

Kwa maana ni nani ajuaye yaliyo mema ya mwanadamu katika maisha yake, siku zote za maisha yake ya ubatili, anayoishi kama kivuli? Kwa maana ni nani awezaye kumweleza mwanadamu mambo yatakayofuata baada yake chini ya jua? Mhubiri 6:12

For who knows what is good for man in life, all the days of his vain life which he spends like a shadow? For who can tell a man what will be after him under the sun?